Habari mwanajumuiya ya Ngudu sekondari tunayo furaha kubwa sana kukufahamisha kuwa sasa shule yetu imefungwa kwa ajili ya likizo fupi ya April na wanafunzi wote wameruhusiwa kuanza likizo hiyo wakiwa nyumbani na wazazi wao.
Mkuu wetu mpya wa Shule ndugu HENRY M. GABRIEL alitumia nafasi hiyo kutoa usia kwa wanafunzi wote katika mkusanyiko mdogo wa Baraza la shule.
Miongoni mwa mambo muhimu sana aliyosisitiza ni kuwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii sana ili kuongeza ufaulu wa wao.
Na kwa kutekeleza hilo kuna walimu wamejitolea kuendelea kufundisha kwa wakati wote wa likizo ili kufanikisha zoezi hilo. Tunawaomba wazazi kuwaruhusu watoto hao kurudi shuleni kwa ajili ya programu hiyo.
Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo;
Baada ya kusema hayo mkuu alifunga shule mpaka baada ya wiki mbili kuanzia sasa tar. 06/04/2017
Asante na karibu ngudu sekondari.
Imeandikwa na PIUS JUSTUS MULIRIYE
0 comments:
Post a Comment