KARIBU NGUDU SECONDARY

KARIBU NGUDU SECONDARY
Searching...
Wednesday, March 8, 2017

RISALA YA SHULE KWA MGENI RASMI NA WAZAZI KWENYE MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA SITA, March 3, 2017

4:05 AM

RISALA YA SHULE KWA MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI YA 11 YA KIDATO CHA SITA, March 3, 2017
Mheshimiwa Mgeni Rasmi;
Mh; JOHN C. KIMASA
Diwani wa kata ya Ngudu.
Waheshimiwa Mjumbe wa Bodi ya Shule,
Waheshimiwa Wageni Waalikwa,
Waheshimiwa Wapendwa Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wote,
Waheshimiwa Walimu, wafanyakazi na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngudu,
Mabibi na mabwana.
Mheshimiwa mgeni rasmi;

Awali ya yote kwa niaba yangu na kwa niaba ya jumuiya yote ya ngudu sekondari, napenda kukushukuru wewe binafsi, wageni waalikwa, wazazi wa wanafunzi wetu kwa kuacha shughuli zenu nyingi na muhimu ili mjumuike nasi katika hafla hii ya kuwaaga wanafunzi wetu wa kidato cha sita 2017. Kwa tendo hilo nasema asanteni sana kwa kufika kwenu kwani hii ni alama ya upendo wenu kwa shule hii.

Mheshimiwa mgeni rasmi

Ni wazi kabisa tukushukuru mheshimiwa mgeni rasmi kwa moyo wako wa upendo unaonesha kwetu, umekuwa ukitutembelea mara kwa mara, hii inaonesha uko pamoja na sisi. Hongera sana.

Mheshimiwa mgeni rasmi;
Shule ya ngudu sekondari ilianza mwaka 1989 ikiwa na kidato cha kwanza tu, na kidato cha tano kilianza mnamo mwaka 2005. Mahafali haya ni ya 11 tangu kidato cha tano kuanzishwa.

Mheshimiwa Mgeni rasmi;
Shule yetu ya Ngudu sekondari inao wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita kama ifuatavyo:-

O’LEVEL
ME
KE
JUMLA
289
284
573
A’LEVEL
360

360
J/KUU
649
284
933


Mheshimiwa mgeni rasmi; miundombinu upande wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za walimu ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini;



MAHITAJI
YALIYOPO
PUNGUFU
VYUMBA VYA MADARASA
24
20
04
MATUNDU YA VYOO VYA WANAFUNZI
ME
26
06
20
KE
14
06
08
NYUMBA ZA WALIMU
         63
09
54

Mheshimiwa mgeni rasmi, ifuatayo ni takwimu ya idadi ya walimu tulionao katika shule yetu. Jedwali hapo chini linaonyesha idadi ya walimu hao.


SANAA
ME
KE
JUMLA
27
21   
48
SAYANSI
12
  3
15
J/KUU
41
22
63

1.      Mheshimiwa mgeni rasmi;
Shule yetu ina wanafunzi kidato cha kwanza hadi cha sita katika michepuo ya sanaa na sayansi yaani HKL, HGL, HGK, PCB, PCM,na CBG

Mheshimiwa mgeni rasmi, matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha 2, 4 na 6 yanaweza kutupa picha ya maendeleo ya taaluma katika shule yetu kama ifuatavyo.

A: KIDATO CHA PILI 2012-2916


2012

56%


A
B
C
D
F

KE
0
0
9
24
45

ME
0
6
25
29
26


0
6
34
53
71

2013

43.6%

A
B
C
D
F

KE
0
1
6
13
61

ME
1
14
19
29
46


1
15
25
42
107

2014

92%
JINSI
DARAJA I
DARAJA II
DARAJA III
DARAJA IV
FLD

KE
01
05
08
51
06

ME
09
10
08
36
05

JML
10
15
16
87
11


2015

89.69%

SEX
DARAJA I
DARAJA II
DARAJA III
DARAJA IV
FLD
KE
0
05
05
27
06
ME
04
07
13
26
04

JML
04
12
18
53
10







2016
SEX
I
II
III
IV
FLD
KE
2
2
8
46
4
ME
8
10
9
30
4
JML
10
12
17
76
8

B: KIDATO CHA NNE 2012-2016

2009
DARAJA


I
II
III
IV
FLD
PASS%
03
11
37
113
54
75.2
2010
I
II
III
IV
FLD


03
09
14
67
52
64.1
2011
I
II
III
IV
FLD


0
03
09
86
75
56.6
2012
I
II
III
IV
FLD


0
02
07
70
113
41.1








2013
I
II
III
IV
FLD
PASS%
0
08
20
69
65
59.8







2014
I
II
III
IV
FLD
PASS%
02
08
18
39
18
75







2015
I
II
III
IV
FLD
PASS%
01
15
08
60
55
60







2016
I
II
III
IV
FLD
PASS%
0
07
15
50
54
57







C: KIDATO CHA SITA 2012-2016

2011
DARAJA

PASS%
I
II
III
IV
FLD


09
35
73
20
08
94.1
2012
02
17
97
26
08
94.6
2013
01
09
92
20
05
96.1
2014
07
28
72
24
04
97.1
2015
15
35
83
24
02
98
2016
11
75
76
10
01
99.4%




Mheshimiwa mgeni rasmi;
Mheshimiwa mgeni rasmi;
Shule ina mpango wa kuboresha ufaulu wa shule. Tunaomba wazazi washirikiane na walimu kusisitiza yafuatayo;
Ø  Kwa pamoja tusisitize utii na nidhamu kwa ujumla.
Ø  Tusisitize wanafunzi wafike shuleni kila siku na wawepo shuleni wakati wote.
Ø  Tunatafuta njia endelevu za kuwatambua wenye vipaji maalum pamoja na wale wanaofanya vizuri darasani ikiwa ni pamoja na walimu wanaotimiza wajibu wao kitaaluma wapewe zawadi ikiwa ni mbinu endelevu ya kuboresha taaluma.

Mheshimiwa mgeni rasmi;
Shule yetu imekuwa ni miongoni mwa shule zinazojitahidi kufanya vizuri kulingana na uhalisia wa wanafunzi tunaopokea kujiunga kidato cha kwanza, kwani wengi wao hawana wastani unaoridhisha kujiunga na kidato cha kwanza.

Kwa mfano; wanafunzi wa kidato cha nne 2016 tuliwapokea wakiwa chini ya wastani ambapo wanafunzi 117 kati ya wanafunzi 186 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza walikuwa chini ya alama 100. Waliostahili kujiunga kidato cha kwanza ni wanafunzi 69 tu kwa sifa zinazotumiwa (kuanzia alama 100 na kuendelea).

Shule yetu pia imefanikiwa kufungua tovuti ambayo wazazi na wadau wa elimu katika shule yetu, watakuwa wakipata taarifa za shule ikiwemo matokeo ya wanafunzi, fomu za kujiunga na kidato cha kwanza na cha tano n.k.
Tovuti hiyo inapatikana kwa kubonyeza www.ngudusecondary.com katika simu yako au kompyuta yako.

Mheshimiwa mgeni rasmi; Pamoja na mafanikio hayo, shule yetu ina changamoto mbalimbali kama ifuatavyo;
·         Upungufu mkubwa wa walimu katika masomo ya sayansi kwa vidato vyote 1-6, ambapo kuna upungufu wa walimu wapatao 15. Hii inawalazimu walimu wa sayansi waliopo wafundishe kuanzia kidato cha 1-6. Hali hii inasababisha walimu hawa kutomaliza baadhi ya mada kwa baadhi ya madarasa na hivyo kusababisha kutokuwa na ufaulu mzuri wa wanafunzi katika masomo ya sayansi.
·         Upungufu wa vyumba vya madarasa unaopelekea kuunganisha mikondo miwili  au mitatu kwenye chumba kimoja, hali inayosababisha changamoto ya kulitawala darasa.
·         Ukosefu viti na meza 63 kwa walimu, hii inasababisha walimu washindwe kupata mahali salama na pa kuandalia masomo kwa ajili ya kufundishia.
·         Upungufu wa nyumba za walimu, ambapo tuna upungufu wa nyumba 54 kati ya 9 zilizopo.

Mheshimiwa mgeni rasmi; tunakushukuru kwa namna unavyoendelea kutoa msukumo kwa halmashauri yetu kuhakikisha matatizo ya shule yetu yanatatuliwa. Kwa mfano; mwezi februari shule imepokea shilingi milioni mbili za kuendeleza ujenzi wa vyoo.
Tunaomba kwa msukumo huohuo uendelee kutusaidia upatikanaji wa samani za shule hasa viti na meza za walimu, vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu


Mheshimiwa mgeni rasmi; Mwisho wa sherehe hii tutakuomba utoe vyeti na zawadi kwa wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita 2017.

Na pia tunakuomba utoe nasaha zako kwa wanafunzi hawa ukiwa ni mwanga kwa maisha yao ya baadaye.
            Asante sana,



…………………………………
JOHN .C. KIMASA.


1 comments: